wahusika wetu

wapiga kura vijana

Vijana ambao hawana (au wamepoteza) msisimko wa maswala ya siasa.

wagombea vijana

Vijana wanaotamani kuwa viongozi ili wasimamie maswala ya vijana.

wanahabari vijana

Vijana wenye weledi, wanaotamani kuuhabirisha uma kuhusu uchaguzi.

Nini chanzo

Tunataka kufanya upigaji kura, siasa na majadiliano ya kiraia kuwa masuala yenye kipaumbele kwa vijana na sehemu ya tamaduni ya kisasa ya Kitanzania.

Wadau wetu

 • Vijana
 • Mashirika ya Vijana
 • Vyama vya siasa
 • Wagombea vijana
 • Vyombo vya Habari
 • Serikali ya Tanzania

Mipango yetu

Uchaguzi 2020 tunataka kusababisha kihivi.

 • Kuanzisha jukwaa la habari mtandaoni

  Kujenga jukwaa la habari la mtandaoni 'Kijana Voice' kuunganisha vijana wa kitanzania.

 • Kuwafikia angalau vijana milioni 10

  Kufikia vijana milioni 10 kupitia mitandao ya jamii, vyombo vya habari na mitaani.

 • Kuhusisha mashirika 50 ya vijana

  Kushirikisha mashirika 50 ya vijana kukagua na kukuza Ilani ya vijana.

 • Kuajiri washawishi 100 wa mtandaoni

  Kuajiri washawishi 100 wa mitandao ya kijamii kuendesha kampeni ya Kura Yetu.

 • Kuwezesha wagombea 200

  Kusaidia wagombea 200 vijana walio tayari kugombea.

 • Kutumia waangalizi 3000 wa uchaguzi

  Kushirikisha waangalizi vijana wa uchaguzi 3000 kutoka kanda 6.

 • Kuwawezesha waanahabari 50

  Kuwawezesha waandishi wa habari vijana 50 kutoa taarifa za uchaguzi.