Jiandikishe kupiga kura

Ikiwa wewe ni raia wa kitanzania, una umri wa miaka 18 au zaidi na unastahili kupiga kura kulingana na Katiba na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi (2010) pamoja na sheria zingine zilizotungwa na bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania; yaani, una akili timamu na haujahukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi sita au kupewa hukumu a kifo na mahakama basi huna sababu ya kutojiandikisha kupiga kura.

Nenda          
kapige kura

Umeshajisajili kupiga kura? Chukua hizi 👊
Sasa fuata muongozo ufuatao ili uweze kupiga
kura ifikapo siku yenyewe.

 1. Hakiki jina lako Hakikisha ikiwa jina lako liko kwenye orodha ya wapiga kura mara tu itakapotolewa kwa umma
 2. Fahamu kituo chako Fahamu kilipo kituo chako cha kupigia kura kwa kupitia jina lako katika orodha itakayotolewa na NEC
 3. Wajue wagombea Tambua ni mgombea gani unayempigia kura kwa kufuata kampeni za uchaguzi kwa karibu
 4. Usifanye kampeni muda ukiisha Usishiriki kampeni yoyote ya uchaguzi siku moja kabla ya uchaguzi mkuu
 5. Usifanye uchochezi kituoni Usivae mavazi ya vyama vya siasa kwenye vituo vya kupiga kura
 6. Nenda na washkaji Usiende peke yako! hamasisha vijana wenzako mkapige kura pamoja
 7. Usisahau kadi yako Kabla hujatoka nyumbani hakikisha umechukua kadi yako ya mpiga kura
 8. Cha muhimu amani Piga kura kwa amani, na baada ya hapo nenda nyumbani

#TayariKugombea

Je wewe ni kijana wa kitanzania unaependa kuleta mabadiliko chanya kwa kugombea nafasi za serikali? Jiunge na kampeni yetu ya #TayariKugombea upatiwe msaada wa kiustadi, kupewa ushauri na kufundishwa mbinu

Niko Tayari Kugombea
 • Ajira za vijana
 • Elimu Bora
 • Huduma bora za kiafya
 • Utawala bora na uwajibikaji
 • Ushiriki wa Vijana katika nafasi za kimaamuzi

Ibua maswala ya vijana

 • Vijana na Maliasili
 • Michezo, Sanaa, Viwanda na ubunifu
 • Vijana wenye Ulemavu
 • Vijana na diplomasia
 • Usawa wa kijinsia

Ibua maswala ya vijana

 • 1 Ajira za vijana
 • 2 Elimu Bora
 • 3 Huduma bora za kiafya
 • 4 Utawala bora na uwajibikaji
 • 5 Ushiriki wa Vijana katika nafasi za kimaamuzi
 • 6 Vijana na Maliasili
 • 7 Michezo, Sanaa, Viwanda na ubunifu
 • 8 Vijana wenye Ulemavu
 • 9 Vijana na diplomasia
 • 10 Usawa wa kijinsia

fuatilia wagombea

Jenga Jimbo ni jukwaa la kimtandao ambalo litawawezesha raia kuripoti adha wanazopata mitaani moja kwa moja hadi kwa serikali za mitaa. Utaweza kushiriki jukwaa hili kupitia app na tovuti. Vyote vinafanyiwa kazi na vitakujia hivi karibuni.